Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)
Je, UndaCV ni bure?
Ndio! UndaCV ni bure kabisa. Hakuna malipo yoyote, hakuna akaunti inayohitajika, na hakuna gharama
za siri.
Je, data yangu ni salama?
Kabisa! Taarifa zako zote zinahifadhiwa kwenye kivinjari chako tu (localStorage). Hatutumi data yako
kwenye seva zetu, kwa hiyo ni salama 100%.
Ninaweza kutengeneza CV ngapi?
Unaweza kutengeneza CV nyingi kadri unavyotaka! Hakuna kikomo cha idadi ya CV unazoweza kuunda.
Je, CV yangu itakubaliwa na waajiri?
Ndio! CV zetu ni ATS-friendly (zinapita kwenye mifumo ya kuchuja wafanyakazi) na zina muundo wa
kitaalamu unaokubaliwa na waajiri wengi.
Ninaweza kutumia kwenye simu?
Ndio! UndaCV inafanya kazi vizuri kwenye simu, kompyuta, na tablets. Unaweza kutengeneza CV yako
popote.
Kama nina tatizo, ninaweza kupata msaada wapi?
Tuandikie barua pepe kwa support@undacv.com au tumia fomu ya mawasiliano hapo juu. Tutajibu ndani ya
masaa 24.